Usajili washika kasi mkoa wa Arusha, waandishi kutoka vyombo vya habari watembelea vituo vya Usajili

Baadhi ya waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari zikiwemo Televisheni na Magazeti Jana walitembelea vituo vya Usajili mkoa wa Arusha kuona hatua za usajili na mwitikio wa wananchi katika kupata haki yao msingi ya kikatiba ya kusajiliwa.

Wananchi wa Mkoa wa Arusha wameendelea kujitokeza kwa wingi kujisajili Vitambulisho vya Taifa; huku idadi ya Kata za Usajili zikiongezeka. Moja ya Kata iliyoanza Usajili jana kwa upande wa Wilaya ya Arusha mjini inaendelea kuwasajili wananchi katika Kata ya Themi, Sekei, Sombetini na wameongeza Kata nyingine ya Sinoni.

Wilaya ya Monduli inakamilisha usajili kwenye Kata za Monduli Mjini, Monduli Juu na Engutoto; ikijipanga kuendelea na Kata za Lashaine, Sepeko, Meserani na Mfereji.  Kwa Upande wa Arumeru Kata zinazofanya Usajili ni Musa, Ambureni, Leburuki, Imbasenyi na Ngabobo, Longido ni Kata za Olubomba, Namanga na Kimokoa na wanajiandaa na Kata za Kamwanga, Tingatinga, Olumorodi na Sinya. Karatu wanaendelea na Usajili kwenye Kata ya Karatu na Rhotia kabla ya kuhamia Ganako. Wilaya ya Ngorongoro wameanza na Tarafa ya Ngorongoro kabla ya kuanza Mitijo.

Uongozi wa Mkoa umejizatiti kuhakikisha wananchi wote wanasajiliwa kwa wakati na kupata Vitambulisho vya Taifa vitakavyowawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali pamoja na upatikanaji kirahisi wa huduma za kijamii.

 

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (NIDA) Bi. Rose Joseph (mwenye miwani) akizungumza na baadhi ya waandishi wa Vyombo vya Habari vya Televisheni na Magazeti walipotembelea kituo cha usajili cha Sombetini, Arusha mjini kuangalia shughuli za kuwasajili wananchi zinazoendelea kituoni hapo.

 

Wananchi wakiendelea kupata huduma za usajili kabla ya kupigwa picha kama wanavyoonekana pichani. Wananchi hao ambao ni kutoka Kata ya Sombetini wamekuwa wakijaziwa fomu na kugongewa mihuri na wenyeviti kwenye mitaa wanayoishi kabla ya kusajiliwa kwenye mfumo wa NIDA.

 

Hapa ni Mwenyekiti wa mojawapo ya mitaa ya Kata ya Sombetini (mwenye kofia) akigonga mhuri kwenye fomu ya mwananchi kuthibitisha kumtabua, na mkazi wa eneo lake.

 

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Sinoni Arusha wakiwa kwenye foleni ya kupigwa picha baada ya kukamilisha hatua za awali za Usajili ambazo ni kujaza fomu za maombi na kuthibitishwa na Idara ya Uhamiaji.

 

Moja ya mashine aina ya BVR ikiendelea kuwasajiliwa wananchi wa Kata ya Sinoni waliopanga foleni kupata huduma ya Usajili.

Akina mama pamoja na jukumu la malezi wamejitokeza kusajiliwa kama anavyoonekana pichani mmoja wa akinamama wa Kata ya Sinoni akiwa amembeba mtoto wake mkono mmoja na mkono mwingine akiwa anaendelea na hatua za usajiliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Namba za vitambulisho zilizotengenezwa

Tarehe idadi
10 August 2016 (....)

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu