Usajili Vitambulisho vya Taifa waendelea mkoa wa Geita

Wananchi wa Halmashauri ya mji Geita, mkoani Geita wameendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la usajili na utambuzi linaloendeshwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa. Zoezi hili ambalo kwa sasa linaendelea mikoa yote ya Kanda ya Ziwa na Kaskazini limekuwa ni fursa nzuri na muhimu kwa wananchi  kusajiliwa na kuwezeshwa kushiriki katika shughuli za maendeleo kutokana na umuhimu wa taarifa zinazokusanywa.

Pindi mfumo huu utakapokamilika wananchi watawezeshwa kupata huduma mbalimbali kwa urahisi pamoja na kusaidia Serikali kuimarisha Ulinzi na Usalama wa nchi kwani Kitambulisho hiki kitakuwa ufunguo kwa mifumo mingine ya Serikali kubadilishana taarifa.

 

Wananchi kata ya Bulela Halmashauri ya Mji Geita wakisubiri huduma ya usajili wakati wa zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea  Mkoani Geita.

 

Afisa Msajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, akiendelea na zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa kwa Wananchi wa mtaa wa Station kata ya Mtakuja Halmashauri ya Mji Geita.

 

Wananchi wa mtaa wa Station kata ya Mtakuja Halmashauri ya Mji Geita katika foleni wakisubiri kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa, wakati wa zoezi la usajili linaloendelea mkoani humo.

 

Maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakiendelea na zoezi la uingizaji wa taarifa za wananchi katika zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa linaloendelea katika Halmashauri ya Mji Geita Mkoani Geita.

 

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uratibu Ofisi za wilaya Bi. Rehema Kionaumela akitoa maelekeza kwa Maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Mkoani Geita kuhusu taratibu mbalimbali wakati wa maandalizi ya zoezi la usajili  wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji Geita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Namba za vitambulisho zilizotengenezwa

Tarehe idadi
10 August 2016 (....)

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu