Zoezi la Usajili na Utambuzi laanza rasmi mkoani Singida

Katika kufanikisha Lengo Msingi la Serikali la kuwasajili na kuwatambua Wananchi wake wote, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa – NIDA kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida imezindua zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu Mkoani humo lenye lengo la kuwasajili Wananchi wote waliofikisha Umri wa Miaka 18 na kuendelea,pamoja na Wageni wakaazi na Wakimbizi waliotimiza Vigezo na Masharti ya kupatiwa kitambulisho cha Taifa kitakachowatambulisha kila mmoja kwa hadhi ya Uraia wake.

Akizindua zoezi hilo Mkuu wa Wilaya hiyo amesisitiza Wananchi pamoja, Watendaji wa Serikali za Mitaa, pamoja na Halamshauri za Wilaya kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kupata taarifa sahihi za watu zitakazotumiwa na mifumo yote ya Serikali na binafsi kubadilishana taarifa kwa lengo la kuboresha Huduma na kuinua hali za watu kutoka kipato cha chini kwenda cha Kati.

Akiainisha umuhimu wa zoezi hilo Mkuu huyo wa Wilaya ametaja baadhi ya faida za Vitambulisho vya Taifa ambazo ni Kuimarisha ulinzi na usalama wa Nchi hususan maeneo ya mipakani, Wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji Mali hususani Biashara, usalama katika miamala ya kibenki pamoja na kuwezesha wananchi kukopesheka kirahisi, Upatikanaji kirahisi wa pembejeo na zana za Kilimo, na Wananchi katika Kaya maskini kutambulika haraka na kupata misaada kupitia TASAF.

Aidha ametahadharisha wananchi na viongozi kila mmoja kwa nafasi yake  kukemea kwa vitendo viashiria vyote vya Rushwa, ama udanganyifu utakaofanywa na wachache wasioitakia mema Nchi yetu kwa kuzorotesha zoezi hilo, akiwataka  wananchi kutoa taarifa sahihi na ushirikiano wa karibu kwa viongozi, Wataalamu na wasimamizi wa zoezi hilo waliokasimishwa jukumu la usajili.

Zoezi hilo linalotegemewa kutekelezwa katika awamu nne ambapo katika awamu ya kwanza utekelezaji wake utakuwa katika Tarafa ya Ikungi yenye Kata sita kwa wananchi wapatao 45,599, Awamu ya Pili itakuwa ni Tarafa ya Sepuka yenye Kata Saba na wananchi wakiwa Ni 49,035, Awamu ya Tatu Ni Tarafa ya Ihanja yenye Kata nne huku wananchi wakiwa 54,887 na awamu ya nne itakuwa katika Tarafa ya Mungaa yenye Kata Saba na jumla ya wananchi wapatao 35,311.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mh. Miraji Jumanne Mtaturu akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Usajili Mkoa wa Singida Bi. Agness Mtei, Katibu tawala Winfrida Funto, anayefata ni Mwenyekiti wa Halmashauri Bw. Abel Suri, Madiwani, Wenyeviti pamoja na Watendaji wa kata na Vijiji baada ya kukamilisha uzinduzi wa zoezi la Usajili na Utambuzi wa Wananchi Mkoani Singida.

 

Afisa usajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Mkoani Singida Bi. Agness Mtei na Bi. Shufaa Issa Wakimuelekeza Mh. Mtaturu Mkuu wa Wilaya ya ikungi namna Mfumo wa Usajili na Utambuzi wa watu unavyofanya kazi ikiwemo namna ya kuingiza taarifa pamoja na kuchukua alama za kibaiologia za muombaji wa Kitambusho cha Taifa.

 

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mh. Miraji Mtaturu akisalimiana na baadhi ya Wageni na Wananchi waliohudhuria uzinduzi Rasmi wa zoezi la Usajili na Utambuzi wa Vitambulisho vya Taifa Mkoani Singida ulifanyika katika kata ya Dung’unyi ambapo zoezi la usajili lilikuwa likiendelea.

 

Afsia usajili Vitambusliho vya Taifa – NIDA Bi. Agness Mtei Mh. akifurahia jambo na Mh. Miraji Mtaturu baada ya kumkaribisha Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi aliyekuwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa zoezi la Usajili na Utambuzi linaloendela hivi sasa Mkoani Singida.

 

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mh. Miraji Mtaturu akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Usajili Mkoa wa Singida Wilaya ya Ikungi Bi. Agness Mtei, Dorice Niyukuri, Marry Maputa pamoja Bi. Shufaa Isaa baada ya kuelekezwa namna mifumo ya usajili na Utambuzi inavyofanya kazi katika Uzinduzi wa zoezi la Usajili Mkoani Singida.

 

Wananchi wa kata ya Dung’unyi wakimsikiliza kwa Makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mh. Miraji Mtaturu alipokuwa akizungumza nao wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Usajili na Utambuzi linaloendelea Mkoani Singida.

 

Mh. Mtaturu akiangalia namna mfumo wa Usajili unavyofanya kazi ya kuchukua alama za vidole (Finger Prints) za muombaji wa kitambulisho cha Taifa wakati uzinduzi wa zoezi la usajili uliohusisha uchukuaji wa alama za kibaiologia, saini ya kielektroniki pamoja na picha ya muombaji wa kitambulisho cha Taifa linaoendelea Mkoani Singida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Namba za vitambulisho zilizotengenezwa

Tarehe idadi
10 August 2016 (....)

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu