Tanzia: Tangazo la kifo cha Mtumishi Digna Baltazar Mallya

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ndugu Andrew W. Massawe anasikitika kutangaza kifo cha mtumishi Digna Baltazar Mallya (Afisa Usajili) kilichotokea ghafla Jumamosi 26/08/2017.

Marehemu atasafirishwa kwa mazishi mkoani Kilimanjaro wilayani Rombo, Jumatano 30/08/2017

NIDA tunatoa pole za dhati kwa muwe wa marehemu, watoto, wazazi, ndugu na marafiki wote walioguswa na msiba huu mzito. Kabla ya umauti marehemu alikuwa akifanya kazi ofisi ya Usajili  Wilaya ya Kinondoni. Tutakukumbuka kwa ucheshi wako, uchangamfu na moyo wa kujituma. Mwenyezi Mungu akupokee na akupumzishe kwa amani. AMINA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Namba za vitambulisho zilizotengenezwa

Tarehe idadi
10 August 2016 (....)

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu