Mkuu wa mkoa wa Iringa ameahidi mkoa wake kumaliza usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi ndani ya siku 60.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Juma Masenza; amemhakikishia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Ndugu Andrew W. Massawe mkoa wake kumaliza ndani ya siku 60 zoezi la kuwasajili wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wanaishi mkoani humo.

Ahadi hiyo ameitoa leo alipofanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, wakati alipomtembelea ofisini kwake makao makuu ya mkoa huo yaliyopo Iringa; ikiwa imesalia siku moja kabla ya kufanya uzinduzi rasmi wa kuanza kuwasajili wananchi katika Wilaya zote za Mkoa wa Iringa.

Akifafanua kwanini Mkoa wa Iringa umeamua kuwasajiliwa wananchi wake wote kupata Vitambulisho vya Taifa; Mkuu huyo wa Mkoa amesema mafanikio makubwa ya zoezi la kuwasajili watumishi wa Umma ni moja ya kichocheo kikubwa cha mkoa wake kuona umuhimu kuwatambua wananchi wake wote ili kuwa na idadi sahihi ya wakazi wa mkao wa Iringa; zoezi linaloenda sambamba na kuwasajili wageni wanaoishi kihalali nchini.

kama Mkuu wa Mkoa nimejifunza na kutambua umuhimu mkubwa sana wa Vitambulisho vya Taifa kwa mtu binafsi lakini pia kwa maendeleo ya mkoa, hivyo sioni sababu kwanini tusitumie fursa iliyopo kuwasajili wananchi wetu wakati uwezo wa kufanya hivyo tunao alisitiza.

Kabla ya kutembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA alifanya ziara kutembelea Wilaya ya Kilolo na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Asia Juma Abdallah ambaye alimhakikishia mkurugenzi huyo ushirikiano katika kufanikisha zoezi hilo.

Naye Mwenyekiti ya Halmashauri ya Kilolo Mhe. Mwl. Valence Kihwaga amesema Waheshimiwa Madiwani wako tayari kushiriki katika zoezi hilo na wamejipanga katika kuhakikisha wananchi wao wanapata huduma hiyo.

Mkoa wa Iringa umepanga kufanya rasmi uzinduzi wa kuanza kwa zoezi la kuwasajili Vitambulisho vya Taifa, Wananchi wa mkoa wa Iringa pamoja na kuanza utoaji Vitambusho vya Taifa kwa wananchi katika Wilaya ya Mufindi.

Katibu Tawala katika Mkoa huo amethibitisha tukio hilo na kuanisha mipango ambayo itatumika katika kuhakikisha wananchi wote wanasajiliwa katika kipindi cha siku 60 zilizobainishwa na Uongozi wa Mkoa.

 

Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza, akifanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Ndugu Andrew W. Massawe, wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa makao makuu ya mkoa huo.

 

Mkuu wa Mkoa wa Iringa akiagana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA.

 

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Juma Masenza akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA walipotembelea ofisi yake. Katikati ni Mkuu wa Mkuu wa Mkoa, akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA katikati kulia. Na wa kwanza kulia ni Ndugu Alphonce Malibiche Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa NIDA na wa kwanza kulia ni Bi. Rose Mdami Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati.

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ndugu,  Andrew W. Massawe akifafanua jambo wa Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Juma Abdallah wakati wa alipotembelea ofisi ya Mkuu huyo wa Wilaya Kilolo – Iringa

 

Katika majadiliano ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo Mhe. Mwl. Valence Kihwaga na ujumbe wake wakizungumza na ujumbe wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA kwenye makao makuu ya Halmashauri hiyo – Kilolo

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu akizungumza na watumishi wa NIDA wanaofanya kazi katika Ofisi ya Wilaya ya Kilolo – Iringa 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Namba za vitambulisho zilizotengenezwa

Tarehe idadi
10 August 2016 (....)

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu