Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa yashauriwa kuhamasisha matumizi ya vitambulisho vya taifa katika huduma nchini

Maonesho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yameendelea leo kwenye viwanja vya Maisara – Zanzibar, ambapo wananchi wameendelea kumiminika kwa wingi kwenye banda la maonesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kusajiliwa, kuchukua vitambulisho vyao na kupata elimu kuhusu umuhimu na faida za Vitambulisho vya Taifa.

Miongozi mwa wageni waliotembelea banda hilo ni Mhe. Mwinyiusi A. Hassan, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A”, Dr. Hamed Rashid Hikmany; Mkuu wa chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait Memorial, ambao wamepongeza kazi nzuri inayofanywa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa na kupendekeza Vitambulisho vya Taifa kuanza kutumika katika shughuli mbalimbali ili kupunguza utitiri wa vitambulisho.

“Tuimarishe utendaji na tufanye kazi kwa malengo na kwa kufanikisha utendaji kwa kuendelea kuwa karibu zaidi na Serikali za Wilaya, Shehia na wananchi” alisisitiza Mkuu wa Wilaya.

Aidha; Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Dr. Andrew W. Massawe naye amejumuika na wananchi wa Zanzibar kwa kutembelea na kukagua shughuli zinazofanyika kwenye banda la NIDA Maisara- Zanzibar na kushiriki kuzungumza na kujibu hoja za wananchi wa Zanzibar walio kuwepo kwenye banda la NIDA kupata huduma. Wananchi hao wameonyesha kufarijika na utendaji wa Mkurugenzi huyo na kuelekeza furaha yao kwa jinsi alivyojitoa na kushirikiana na wafanyakazi wake katika kujibu hoja mbalimbali za wananchi.

Akizungumza wakati akijibu hoja za wananchi, Bwana Masssawe amepongeza wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye banda la NIDA kupata huduma na ufafanuzi kuhusu Vitambulisho vya Taifa; na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi kwa jumla kwa kutimiza miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

NIDA tunaahidi kuendelea kuwa karibu zaidi na wananchi kwa kuendelea kutoa huduma nzuri zaidi kwa  wananchi; lengo letu tuhakikishe kila Raia mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea anapata kitambulisho chake, pamoja na kuwasajili Wageni, Wakimbizi wenye sifa za kuishi nchini kama sheria ya Usajili na Utambuzi wa watu inavyoelekeza” Amesisitiza

Maonesho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yalianza tarehe 07 Januari na yatamalizika Jumamosi tarehe 14 Januari 2017 viwanja vya Maisara Zanzibar, NIDA ikiwa miongoni mwa taasisi zinazoshiriki kwa kutoa huduma za Utambulisho kwa wananchi na ugawaji wa Vitambulisho kwa wananchi ambao wamekamilisha taratibu za usajili.

 

Mhe. Mwinyiusi A. Hassan, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A” akiweka saini kwenye kitabu cha wageni alipotembelea banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA kwenye Maonesho ya 53 ya Sherehe za Mapinduzi Zanzibar viwanja vya Miasara Zanzibar. 

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Ndg. Andrew W. Massawe akisaliana na Ndg. Aboubakar Mikidadi Othuman mwananchi aliyetembelea banda la NIDA kupata huduma ya Usajili.

 

Ndg. Abdulaziz Juma Mtumwa (kushoto) Afisa Msajili Msaidizi – NIDA akimsajili  Ndg. Aboubakar Mikidadi Othuman kupata kitambulisho cha Taifa baada ya kupokea maelezo ya kina toka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA.

 

Dr. Hamed Rashid Hikmany; Mkuu wa chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait Memorial akiweka saini kitabu cha wageni alipotembelea banda la maonesho la Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa Zanzibar

 

Mmoja wa wananchi akipata maelezo ya kina kuhusu muonekano mpya wa Kitambulisho cha Taifa alipofika kutembelea banda la NIDA Maisara – Zanzibar.

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Ndg. Andrew W. Massawe akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi kwenye banda la Mamlaka ya Vitambulisho NIDA-  Maisara Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Namba za vitambulisho zilizotengenezwa

Tarehe idadi
10 August 2016 (....)

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu