Wananchi wajitokeza kwa wingi kutembelea banda la maonesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) viwanja vya Maisara – Zanzibar

Wananchi wa Zanzibar leo wamejitokeza kwa wingi kwenye sherehe za uzinduzi wa maonesho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar, yanayoendelea kwenye viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.

Maonesho hayo yamezinduliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa  Dr. Ali Mohamed Shein, ambaye pamoja na mambo mengine amesisitiza Taasisi za Serikali na binafsi kutumia vema fursa ya maonesho kujitangaza na kuonyesha shughuli wanazofanya kwa wananchi.

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ni miongoni mwa Taasisi zinazoshiriki maonesho hayo ambapo pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa Vitambulisho, inaendesha zoezi la kusajili wananchi ambao bado hawajasajiliwa, kugawa vitambulisho vya Taifa kwa wananchi waliokamilisha taratibu za usajili, pamoja na kuonesha mfumo salama (tovuti) inayotumika kusoma taarifa za mtu zilizoko kwenye mfumo kwa njia ya mtandao. Njia hiyo itawezesha wadau mbalimbali kutumia mfumo huo kuhakiki taarifa za mwananchi mwenye kitambulisho kabla ya kumpatia huduma.

Banda la NIDA limekuwa moja ya mabanda ya kuvutia, ambapo wananchi wengi  wamekuwa wakitembelea shughuli mbalimbali zinazoendelea kwenye viwanja hivyo na kuonekana kuridhishwa na huduma zinazotolewa na NIDA.

Maonesho ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yameanza tangu Jumamosi tarehe 07 Januari 2017 yakihusisha Taasisi mbalimbali za Serikali zikiwemo Taasisi za Muungano, mashirika na Taasisi binafsi na yanatarajiwa kumaliza Jumamosi tarehe 14/01/2017.

 

Wafanyakazi wa NIDA wakiwa katika picha ya pamoja, wakijipanga katika Banda la maonyesho hapo katika viwanja vya maonyesho vya Biashara vya Maisara Zanzibar ili kuhudumia wananchi watakaohudhuria.

 

Ofisa wa NIDA Ng Abdulaziz Juma Mtumwa akimkabidhi Dada Lidia Adminic Kaguo Kitambulisho chake katika Banda la Maonyesho wakati maonesho ya sherehe za Mapinduzi Zanzibar yakiendelea kwenye viwanja vya Maisara

 

Kaimu Meneja wa kitengo cha Operesheni Zanzibar Ndg. Abdala O. Mmanga akitoa elimu juu ya matumizi ya Vitambulisho Vya Taifa kwa wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Maonyesho vya Maisara Zanzibar

 

Baadhi ya Wafanyakazi wa NIDA wakifuatilia hutuba ya Mh Raisi wa Zanzibar alipofungua maonyesho ya Biashara ya 3 viwanja vya  Maisara- Zanzibar.

 

Bi. Shau Mwalim Haji akimsajili mwananchi aliejitokeza katika maonyesho ya Biashara ya Maisara.

 

 

Wananchi wakijisajili kwenye kitabu cha wageni walipofika kutembelea banda la Maonesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) viwanja vya Maisara Zanzibar

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Namba za vitambulisho zilizotengenezwa

Tarehe idadi
10 August 2016 (....)

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu