Uzinduzi ugawaji Vitambulisho vya Taifa mkoa wa Arusha

Katibu Tawala Mkoa Ndg. Richard Kwitege amezindua rasmi zoezi la Ugawaji Vitambulisho vya Taifa katika mkoa wa Arusha kwa Watumishi na wananchi waliokamilisha taratibu za usajili.

Akizindua zoezi hilo, Ndugu Kwitege ameishukuru NIDA kwa hatua nzuri waliyopiga na jitihada madhubuti walizozifanya katika kuhakikisha vitambulisho vinaanza kutolewa katika mkoa wa Arusha.

Zaidi ya Watumishi waliosajiliwa 26,000 na kuwaasa watumishi ambao bado kujiandikisha wafanye hivyo mara moja. Amewaasa makundi ambayo yatapatiwa vitambulisho kuvitunza kwani vina matumizi mapana katika katika kupata na kuboresha huduma.

Akizungumzia wananchi Katibu huyo aliwawaasa “wakazi wote wenye sifa za kuweza kusajiliwa waishio mkoani Arusha mjitokeze sasa kwa wingi zoezi la NIDA linapoendekea kwani Vitambulisho vina manufaa makubwa kwa Taifa letu hususani mkoa wetu wa Arusha” Alisisitiza

Mbali na vyombo vya Habari, uzinduzi huo ulishuhudiwa na Maafisa Wasajii wa NIDA kutoka wilaya za Arumeru, Monduli na Arusha pamoja na Watendaji wa ngazi mbalimbali za wilaya na ofisi mbalimbali za umma mkoani humo.

 

Katibu Tawala mkoa wa Arusha (RAS), Ndg. Richard Kwitega akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya zoezi la Usajili wa Watumishi wa Umma lililofanyika mkoani Arusha kuanzia tarehe 03/10/2016 hadi tarehe 31/10/2016

 

Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu kutoka Boari ya Dawa (MSD) Tawi la Arusha Ndg. Denis… akikabidhiwa Kitambulisho cha Taifa na Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Ndg. Richard Kwitega.

 

Ndg. Isdory Pancras, Afisa Usajili Wilaya ya Arumeru akipokea Vitambulisho vya wilaya yake kutoka kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Ndg. Richard Kwitega

 

Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Ndg. Richard Kwitega (katikati mstari wa mbele) katika picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na watumishi wa taasisi mbalimbali za serikali walioko mkoa wa Arusha.

 

Mwakilishi kutoka Ofisi ya Wakaguzi Elimu Kanda ya Kaskazini akikabidhiwa Kitambulisho cha Taifa na Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Ndg. Richard Kwitega.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Namba za vitambulisho zilizotengenezwa

Tarehe idadi
10 August 2016 (....)

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu