Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi atembelea Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Zanzibar

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Yussuf Masauni amesema ni vema kuunganisha mifumo ya Serikali na Mfumo wa Vitambulisho vya Taifa ili kusaidia Serikali kuondokana na kero mbalimbali ikiwemo mishahara hewa.

Hayo ameyasema alipofanya ziara , Ofisi ya Mamlaka ya Vitambulisho Vya Taifa Zanzibar ambapo pamoja na kutembelea shughuli zinazofanywa na ofisi hiyo alipata fursa ya  kuzungumza na Wafanyakazi wanaofanya kazi katika Ofisi kuu iliyopo Kilimani Zanzibar.

Katika ziara hiyo, Mh. Masauni ambaye aliambatana na viongozi na maafisa kadhaa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, alishuhudia shughuli ya Usajili kwa wageni ikiendelea na kukabidhi kitambulisho kwa mmoja wa raia wa nchini Ujerumani   Bi Leonie Schollmeyer ambaye alishakamilisha taratibu zote za usajili, na alifika kituoni hapo kuchukua kitambulisho chake. zoezi la Usajili wa Wageni Zanzibar limeanza tangu tarehe 28/11/2016 na linatazamiwa kumalizika tarehe 06/01/2017.

Mh. Masauni amesema ‘’ni lazima kuwe na utaratibu wa kuweza kuunganisha Kanzi Data za Taasisi mbali mbali zinazofanya kazi Tanzania ili kurahisisha utendaji kazi wa Serikali’’.

Amesema Mfumo wa Taifa wa Usajili na Utambuzi wa Watu una manufaa makubwa katika kupambana na ugaidi wa kimataifa na kupunguza uhalifu nchini. Hii ni kwa sababu taarifa zote za Watanzania, wageni na wasio wageni zitakuwa katika Daftari la kumbukumbu la kielektronikizi ambapo mbali na taarifa za kibaiografia pia taarifa za kibaiolojia zimeunganishwa katika mfumo huo na hivyo kurahissisha zoezi la utambuzi, alisisitiza.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu Zanzibar; Kaimu Mkurugenzi ofisi ya Zanzibar ndugu Hassan Haji Hassan amemweleza Mh. Waziri jitihada zinazofanywa na NIDA katika kuhakikisha watu wote wamesajiliwa ili vitambulisho vya Taifa kuanza kutumika kusaidia Serikali katika kutatua baadhi ya kero za wananchi ikiwa ni pamoja na kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato kwa kuwa watu wake watakuwa wanatambulika.

Mh. Naibu Waziri alihitimisha ziara yake kwa kuwapongeza NIDA kwa kukamilisha zoezi la usajili kwa wananchi wanaoishi katika Wilaya mbali mbali za Zanzibar, ambapo usajili Zanzibar umekamilika kw asilimia 91% .

img1

Mh Naibu Waziri akiwa na Menejimenti ya Ofisi Kuu NIDA Zanzibar.

img2

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Ofisi ya NIDA Zanzibar, wakimsikiliza kwa makini  Mhe. Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi alipotembelea ofisi hiyo

 

img3

Kaimu Mkurugenzi wa NIDA ofisi ya Zanzibar Bw. Hassan Hajji Hassan akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Mh. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

 

img4

Muheshimiwa akipewa ufafanuzi mabali mbali katika chumba cha kuingiza na kuchakata Taarifa

 

img6

Bibi Leonie Schoomeyer akipokea kitambulisho chake cha Taifa kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Namba za vitambulisho zilizotengenezwa

Tarehe idadi
10 August 2016 (....)

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu